Anemia inaweza kukuathiri kwa njia tofauti ikiwemo uwezo wako wa kufanya kazi na kusoma, hedhi yako na mimba za baadaye.
• Utapokea vijalizi vya kawaida kwa wanaougua anemia bili malipo.
• Huenda ukapewa tiba ya utafiti, Asidi ya Tranexamic (TXA).
• Utaombwa kuhifadhi shajara ya afya kuhusu ustawi wako.
• Utahitajika kuhudhuria ziara za utafiti na kupimwa damu.
• TXA tayari inatumiwa kuokoa maisha ya watu ambao wana matatizo makubwa ya uvujaji damu kama vile majeraha, upasuaji mkubwa na baada ya kujifungua.
• TXA haina madhara yoyote makubwa na haijabainishwa kuna na madhara ya kudumu.
• Tunatoa vipimo vya damu bila malipo kuchunguza iwapo mhusika anaugua anemia katika wanawake ambao wana umri wa miaka 18 au zaidi na ambao wanapokea hedhi.
• Ikiwa unaugua anemia, tutakupa fursa ya kushiriki katika utafiti wa kimataifa wa kutafuta njia bora zaidi za kutibu anemia.
