Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

English

Unahisi kuchoka na kuwa na uchovu?

Unaweza kuwa na upungufu wa damu

Shiriki katika utafiti muhimu ili kusaidia kupata njia bora za kutibu upungufu wa damu kwa wanawake. Pima bila malipo na usaidie kuunda mustakabali wa afya ya wanawake.

Jaribio la WOMAN-3.

Haya yote yanahusu nini?

Jinsi utafiti unavyofanya kazi

Kujiunga ni mchakato rahisi wa hatua mbili.

HATUA YA 1

Uchunguzi Bila Malipo

Tunafanya kipimo cha damu cha haraka, kidoleni, bila malipo ili kuangalia upungufu wa damu.

    • Maumivu kidogo ya kidole
    • Maswali mafupi kuhusu afya
    • Fahamu ikiwa una vigezo

HATUA YA 2

Jaribio Kamili

Ikiwa unatimiza vigezo, utapata matibabu ya jaribio kwa vipindi 6 vya hedhi. Pia tutakupa madini ya chuma na vitamini ambayo unaweza kutumia kwa miezi 3.

    • Tumia vidonge wakati wa hedhi
    • Ukaguzi wa mara kwa mara
    • Kuwa na Shajara ya Afya
Kwa nini Ushiriki?

Ushiriki wako utasaidia kupata njia bora za kutibu upungufu wa damu huku ukikupa huduma bora.

Matibabu ya upungufu wa damu bila malipo

Pokea virutubisho vya madini ya chuma na vitamini bila gharama.

Kufidiwa Pesa za Usafiri

Tunalipia usafiri wako kwa ziara zote za utafiti.

Bidhaa za Hedhi Bila Malipo

Imetolewa na timu ya majaribio kwa matumizi ya kibinafsi.

Zawadi ya shukrani

Utapewa zawadi ya shukrani kwa muda wako.

Je, ninatimiza vigezo vya ushiriki?

Kama unahisi una upungufu wa damu au unahisi kuchoka na kuwa na uchovu, unaweza kualikwa kuwa sehemu ya jaribio kamili.

Vigezo vya Ustahiki

√ Wewe ni mwanamke mwenye umri wa miaka 18 au zaidi

√ Unapata hedhi angalau kila baada ya siku 38

√ YHuna ujauzito au huna mpango wa kushika ujauzito kwa muda wote wa jaribio

√ Matibabu ya bure kwa maambukizi yaliyopatikana (kwa baadhi ya washiriki)

√ Kipimo chetu cha bure kinaonyesha kuwa una upungufu wa damu

Kutana na Timu ya Tanzania

Tutafiti wa WOMAN-3 nchini Tanzania unaongozwa na wataalamu walio
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Prof. Projestine Muganyizi

Mratibu Mkuu, Tanzania

Wasiliana na timu ya uratibu ya Kitaifa ya WOMAN-3 ya Tanzania

MAWASILIANO YA ENEO:

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara na Ushauri

Majibu na Suluhisho kwa Maswali Yako

Tayari ninatumia dawa za chuma na asidi ya foliki, nifanye nini?

Unaweza kuendelea kutumia virutubisho vyako vya sasa kwa miezi 3 ijayo, kisha uache kuvitumia kwa kipindi chote kilichobaki cha utafiti. Au, unaweza kutumia virutubisho vitakavyotolewa na utafiti, ambavyo utavitumia kwa muda wa miezi 3 tu. Uamuzi ni wako.

Nianze kujaza daftari langu lini katika kila mzunguko wa hedhi?

Ni vizuri kuanza kujaza daftari lako siku mbili kabla ya tarehe ambayo unatarajia kuanza hedhi. Kulingana na tarehe ya hedhi yako iliyopita, tunaweza kukadiria tarehe ya kuanza hedhi yako inayofuata na kuiandika kwenye daftari lako ili ikukumbushe. Pia tutakutumia ujumbe wa SMS (WhatsApp) au barua pepe kukukumbusha kabla ya tarehe hiyo. Ikiwa hedhi yako itaanza mapema kuliko ulivyotarajia, anza kujaza daftari lako mara tu hedhi yako inapoanza.

Taarifa za Utafiti

Habari za hivi punde kutoka kwenye Utafiti wa WOMAN-3 na kutoka nchini kwako
 

two researchers looking at an Investigational Medicinal Product ready to randomise a participant
Menstrual bleeding in Pakistan: Cultural beliefs add to chronic anaemia in girls and women
By Professor Rizwana Chaudhri, obstetrician, gynaecologist, and National Coordinator for the WOMAN Trials in Pakistan  In my clinical practice in Pakistan, I routinely encounter women who believe that heavy menstrual bleeding is not only normal but desirable. This misconception...
Picture of Dr Abiola Akiyode-Afolabi, founder of the Women Advocates Research and Documentation Center (WARDC)
Challenging discrimination in maternal healthcare: interview with Dr Abiola Akiyode-Afolabi 
10 March 2025. In 2002, Nigerian lawyer and civil rights activist, Dr Abiola Akiyode-Afolabi, founded the Women Advocates Research and Documentation Center (WARDC), with two female lawyers in Nigeria seeking justice to prevent maternal deaths. WARDC primarily provides pro bono legal services...
Haleema-and-Amy-in-scrubs-scaled-1-726x1024
International Clinical Trials Day: how our experts are improving women’s health through inclusion
20 May 2025. To mark International Clinical Trials Day, experts at LSHTM’s Clinical Trials Unit explain why including more women in their work is essential to improving maternal health and women’s health, more generally. Credit: LSHTM.  Professor Nike Bello, WOMAN Trials...

Taasisi Washirika:

Wafadhili Wetu: