English

Ndiyo, kama wewe ni mwanamke:

  • Umri wa miaka 18 au zaidi
  • Una kupata hedhi
  • Una upungufu wa damu. Tutakupima bure ili kujua kama una upungufu wa damu
  • Hujapata mimba na hupangi kupata mimba wakati wa utafiti

Je, naweza kushiriki?

  • Utahitaji kufika mwenyewe kwa ajili ya ziara 4 za ufuatiliaji ili kufanyiwa vipimo vya afya.
  • Utafanyiwa vipimo vya damu mwanzoni na mwishoni mwa utafiti, na utaulizwa maswali kuhusu afya yako na hedhi zako.
  • Utakunywa vidonge mara 3 kwa siku wakati wa hedhi yako kwa siku hadi 5, kwa mfululizo wa hedhi 6 (takribani miezi 6).
  • Utakunywa pia virutubisho vya madini ya chuma (iron) na folic acid kwa miezi 3.
  • Utahitaji kujaza daftari fupi kabla na wakati wa hedhi yako.

Nini nitahitaji kufanya?

Kwa kushiriki, utasaidia kupatikana njia bora zaidi za kutibu upungufu wa damu kwa wanawake kila mahali. Pia unaweza kupata virutubisho bure, vipimo vya afya, na ushauri wakati wa utafiti.

Kwa nini ushiriki?

Sehemu hii itakuwa na taarifa za kukuweka upo-to-date kuhusu maendeleo ya utafiti.
 

Taarifa za utafiti

Hii ni sehemu ya kushiriki taarifa na ushauri wa jumla kwa washiriki, ili kuwasaidia kufahamiana vizuri na taratibu za utafiti wa WOMAN‑3.
 

Ushauri na taarifa nyingine muhimu

Je, unataka kushiriki katika utafiti wa WOMAN‑3?

Tuma barua pepe kwa kituo cha uratibu cha taifa katika nchi yako.