Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

English

Unahisi kuchoka na kuwa na uchovu?

Unaweza kuwa na upungufu wa damu

Shiriki katika utafiti muhimu ili kusaidia kupata njia bora za kutibu upungufu wa damu kwa wanawake.
Pima bila malipo na usaidie kuunda mustakabali wa afya ya wanawake.

 

Jinsi utafiti unavyofanya kazi

Kujiunga ni mchakato rahisi wa hatua mbili.

HATUA YA 1

Uchunguzi Bila Malipo

Tunafanya kipimo cha damu cha haraka, kidoleni, bila malipo ili kuangalia upungufu wa damu.

    • Maumivu kidogo ya kidole
    • Maswali mafupi kuhusu afya
    • Fahamu ikiwa una vigezo

HATUA YA 2

Jaribio Kamili

Ikiwa unatimiza vigezo, utapata matibabu ya jaribio kwa vipindi 6 vya hedhi. Pia tutakupa madini ya chuma na vitamini ambayo unaweza kutumia kwa miezi 3.

    • Tumia vidonge wakati wa hedhi
    • Ukaguzi wa mara kwa mara
    • Kuwa na Shajara ya Afya
Kwa nini Ushiriki?

Ushiriki wako utasaidia kupata njia bora za kutibu upungufu wa damu huku ukikupa huduma bora.

Matibabu ya upungufu wa damu bila malipo

Pokea virutubisho vya madini ya chuma na vitamini bila gharama.

Kufidiwa Pesa za Usafiri

Tunalipia usafiri wako kwa ziara zote za utafiti.

Bidhaa za Hedhi Bila Malipo

Chaguo lako la pedi na bidhaa zingine.

Zawadi ya
shukrani

Ishara ndogo ya shukrani baada ya ziara zako.

Je, ninatimiza vigezo vya ushiriki?

Kama unahisi una upungufu wa damu au unahisi kuchoka na kuwa na uchovu, unaweza kualikwa kuwa sehemu ya jaribio kamili.

Vigezo vya Ustahiki

    √ Wewe ni mwanamke mwenye umri wa miaka 18 au zaidi

    √ Unapata hedhi angalau kila baada ya siku 38

    √ YHuna ujauzito au huna mpango wa kushika ujauzito kwa muda wote wa jaribio

    √ Matibabu ya bure kwa maambukizi yaliyopatikana (kwa baadhi ya washiriki)

    √ Kipimo chetu cha bure kinaonyesha kuwa una upungufu wa damu

Kutana na Timu ya Tanzania

TUtafiti wa WOMAN-3 nchini Tanzania unaongozwa na wataalamu walio Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Prof. Projestine Muganyizi

Mratibu Mkuu, Tanzania

Wasiliana na timu ya uratibu ya Kitaifa ya WOMAN-3 ya Tanzania

MAWASILIANO YA ENEO:

Vidokezi na taarifa nyingine muhimu

Taarifa na usaidizi wa jumla utatolewa hapa ili ujue taratibu za jaribio la WOMAN-3.

Taarifa kuhusu jaribio

Sehemu hii itakuwa na taarifa zitakazokusaidia kufahamu kinachoendelea kuhusu maendeleo ya jaribio.

Taasisi Washirika:

Wafadhili Wetu: